12. Watu wema wakipata madaraka maisha hufana,lakini waovu wakitawala watu hujificha.
13. Afichaye makosa yake hatafanikiwa;lakini anayeungama na kuyaacha atapata rehema.
14. Heri mtu amchaye Mwenyezi-Mungu daima;lakini mkaidi wa moyo ataangukia maafa.
15. Mtawala mwovu anayewatawala maskini,ni kama simba angurumaye au dubu anayeshambulia.
16. Mtawala asiye na akili ni mdhalimu mkatili;lakini achukiaye mali ya udanganyifu atatawala muda mrefu.
17. Mtu anayelemewa na hatia ya kuua mtu,atakuwa mkimbizi mpaka kaburini;mtu yeyote na asijaribu kumzuia.
18. Aishiye kwa unyofu atasalimishwa,lakini mdanganyifu ataanguka kabisa.
19. Anayelima shamba lake atapata chakula kingi,bali anayefuata yasiyofaa atapata umaskini tele.