Methali 27:24-27 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Maana utajiri haudumu milele,wala taji haidumu vizazi vyote.

25. Baada ya kukata nyasi na kuzihifadhi,kata majani toka milimani,huku nyasi zinachipua upya.

26. Kondoo watakupatia sufu kwa mavazi,mbuzi nao utauza na kujinunulia mashamba;

27. watakupa maziwa ya kukutosha wewe na jamaa yako,na kwa ajili ya watumishi wako wa kike.

Methali 27