Methali 26:7-16 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Methali mdomoni mwa mpumbavu,ni kama miguu ya kiwete inayoninginia.

8. Kumpa mpumbavu heshima,ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo.

9. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali,ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi.

10. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi,ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu.

11. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake,ni kama mbwa anayekula matapishi yake.

12. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima?Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.

13. Mvivu husema: “Huko nje kuna simba;siwezi kwenda huko.”

14. Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake,ndivyo mvivu juu ya kitanda chake.

15. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula,lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni.

16. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekimakuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

Methali 26