Methali 26:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake,asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi.

6. Kumtuma mpumbavu ujumbe,ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida.

7. Methali mdomoni mwa mpumbavu,ni kama miguu ya kiwete inayoninginia.

8. Kumpa mpumbavu heshima,ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo.

9. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali,ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi.

10. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi,ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu.

11. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake,ni kama mbwa anayekula matapishi yake.

12. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima?Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.

Methali 26