Methali 26:26-28 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Huenda akaficha chuki yake,lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote.

27. Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe;abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe.

28. Asemaye uongo huwachukia hao anaowaumiza,naye abembelezaye huleta maangamizi.

Methali 26