Methali 26:16-23 Biblia Habari Njema (BHN)

16. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekimakuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

17. Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu,ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita.

18. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge,au mishale ya kifo,

19. ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani,kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!”

20. Bila kuni, moto huzimika;bila mchochezi, ugomvi humalizika.

21. Kama vile makaa au kuni huchochea moto,ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi.

22. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo;hushuka mpaka ndani kabisa tumboni.

23. Kama rangi angavu iliyopakwa kigae,ndivyo yalivyo maneno matamu yenye nia mbaya.

Methali 26