10. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi,ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu.
11. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake,ni kama mbwa anayekula matapishi yake.
12. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima?Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo.
13. Mvivu husema: “Huko nje kuna simba;siwezi kwenda huko.”
14. Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake,ndivyo mvivu juu ya kitanda chake.
15. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula,lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni.
16. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekimakuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
17. Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu,ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita.
18. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge,au mishale ya kifo,
19. ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani,kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!”
20. Bila kuni, moto huzimika;bila mchochezi, ugomvi humalizika.
21. Kama vile makaa au kuni huchochea moto,ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi.
22. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo;hushuka mpaka ndani kabisa tumboni.
23. Kama rangi angavu iliyopakwa kigae,ndivyo yalivyo maneno matamu yenye nia mbaya.
24. Mwenye chuki huficha chuki yake kwa maneno mazuri,lakini huwa ana hila moyoni mwake.
25. Akiongea vizuri usimwamini,moyoni mwake mna chuki chungu nzima.
26. Huenda akaficha chuki yake,lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote.
27. Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe;abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe.