24. Afadhali kuishi pembeni juu ya paa,kuliko kuishi nyumbani pamoja na mwanamke mgomvi.
25. Kama vile maji baridi kwa mwenye kiu,ndivyo habari njema kutoka mbali.
26. Mwadilifu akubaliye kufuata mambo ya mwovu,ni chemchemi iliyochafuliwa au kisima kilichotibuliwa.
27. Si vizuri kula asali nyingi mno;kadhalika haifai kujipendekeza mno.
28. Mtu asiyeweza kuzuia hasira yake,ni kama mji usio na ulinzi unaposhambuliwa.