Methali 24:24-34 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Anayemwachilia mtu mwenye hatia,hulaaniwa na watu na kuchukiwa na mataifa.

25. Lakini wanaowaadhibu waovu watapata furaha,na baraka njema zitawajia.

26. Jibu lililo la haki,ni kama busu la rafiki.

27. Kwanza fanya kazi zako nje,tayarisha kila kitu shambani,kisha jenga nyumba yako.

28. Usishuhudie bure dhidi ya jirani yako,wala usiseme uongo juu yake.

29. Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda!Ni lazima nilipize kisasi!”

30. Nilipitia karibu na shamba la mvivu;shamba la mzabibu la mtu mpumbavu.

31. Nilishangaa kuona limemea miiba,magugu yamefunika eneo lake lote,na ukuta wake wa mawe umebomoka.

32. Nilitazama, nikawaza,mwishowe nikapata funzo:

33. Lala tu kidogo; sinzia tu kidogo!Kunja mikono yako tu upumzike!

34. Lakini kumbuka kwamba uwapo usingizini,umaskini utakuvamia kama mnyanganyi,ufukara kama mtu mwenye silaha.

Methali 24