Methali 22:4-21 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu,utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai.

5. Njia ya waovu imejaa miiba na mitego;anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa.

6. Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri,naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.

7. Tajiri humtawala maskini;mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji.

8. Apandaye dhuluma atavuna janga;uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa.

9. Mtu mkarimu atabarikiwa,maana chakula chake humgawia maskini.

10. Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka,ugomvi na matusi vitakoma.

11. Mwenye nia safi na maneno mazuri,atakuwa rafiki wa mfalme.

12. Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli,lakini huyavuruga maneno ya waovu.

13. Mvivu husema, “Siwezi kutoka nje;kuna simba huko, ataniua!”

14. Kinywa cha mwasherati ni shimo refu;anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo.

15. Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni,lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo.

16. Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe,anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini.

17. Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima,elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu.

18. Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni,na kuyakariri kila wakati.

19. Ninayependa kumfundisha leo ni wewe,ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu.

20. Nimekuandikia misemo thelathini,misemo ya maonyo na maarifa,

21. ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli;na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi.

Methali 22