Methali 22:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Mtu mwangalifu huona hatari akajificha,lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia.

4. Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu,utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai.

5. Njia ya waovu imejaa miiba na mitego;anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa.

6. Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri,naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.

7. Tajiri humtawala maskini;mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji.

8. Apandaye dhuluma atavuna janga;uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa.

9. Mtu mkarimu atabarikiwa,maana chakula chake humgawia maskini.

Methali 22