Methali 22:19-28 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Ninayependa kumfundisha leo ni wewe,ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu.

20. Nimekuandikia misemo thelathini,misemo ya maonyo na maarifa,

21. ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli;na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi.

22. Usimdhulumu maskini kwa kuwa ni maskini,wala usimnyime fukara haki yake mahakamani.

23. Maana Mwenyezi-Mungu atawatetea;atawapokonya maisha yao wale watakaowadhulumu.

24. Usifanye urafiki na mtu wa hasira,wala usiandamane na mwenye ghadhabu,

25. usije ukajifunza mwenendo wake,ukajinasa kabisa katika mtego.

26. Usiwe mmoja wao wenye kuweka ahadi,watu ambao hujiweka wadhamini wa madeni.

27. Ikiwa huna chochote cha kulipa,hata kitanda unacholalia kitachukuliwa!

28. Usiondoe alama ya mipaka ya zamaniambayo iliwekwa na wazee wako.

Methali 22