1. Afadhali kuwa na sifa nzuri kuliko mali nyingi;wema ni bora kuliko fedha au dhahabu.
2. Matajiri na maskini wana hali hii moja:Mwenyezi-Mungu ni Muumba wao wote.
3. Mtu mwangalifu huona hatari akajificha,lakini wajinga hujitokeza mbele wakaumia.
4. Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu,utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai.
5. Njia ya waovu imejaa miiba na mitego;anayetaka kuhifadhi maisha yake ataiepa.
6. Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri,naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.
7. Tajiri humtawala maskini;mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji.