8. Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka,lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka.
9. Afadhali kuishi pembeni juu ya paa,kuliko kuishi nyumbani na mwanamke mgomvi.
10. Anachopania kutenda mtu mbaya ni uovu;hata kwa jirani yake hana huruma.
11. Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima;ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa.
12. Mungu Mwadilifu anajua wanayotenda waovu nyumbani kwao;naye atawaangusha na kuwaangamiza.
13. Anayekataa kusikiliza kilio cha maskini,naye pia hatasikilizwa atakapolilia msaada.
14. Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri;tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu.
15. Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi,lakini watu waovu hufadhaishwa.