Methali 21:2-8 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake,lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo.

3. Kutenda mambo mema na ya haki,humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko.

4. Macho ya kiburi na moyo wa majivunohuonesha wazi dhambi ya waovu.

5. Mipango ya mtu wa bidii huleta mali kwa wingi,lakini kila aliye na pupa huishia patupu.

6. Mali ipatikanayo kwa udanganyifu,ni mvuke upitao na mtego wa kifo.

7. Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali,maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki.

8. Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka,lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka.

Methali 21