Methali 21:13-28 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Anayekataa kusikiliza kilio cha maskini,naye pia hatasikilizwa atakapolilia msaada.

14. Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri;tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu.

15. Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi,lakini watu waovu hufadhaishwa.

16. Anayetangatanga mbali na njia ya busara,atajikuta ametua miongoni mwa wafu.

17. Anayependa anasa atakuwa maskini;anayefikiria tu kula na kunywa hatatajirika.

18. Mwovu atapata pigo ambalo halitampata mtu mwema,mkosefu ataadhibiwa badala ya mnyofu.

19. Afadhali kuishi jangwani,kuliko kukaa na mwanamke mgomvi na msumbufu.

20. Nyumbani kwa mwenye busara mna hazina za thamani,lakini mpumbavu huponda mali yake yote.

21. Anayepania uadilifu na huruma,ataishi maisha marefu na kuheshimiwa.

22. Mwenye hekima aweza kuteka mji wa wenye nguvu,na kuziporomosha ngome wanazozitegemea.

23. Achungaye mdomo wake na ulimi wake,hujiepusha na matatizo.

24. Mwenye majivuno na kiburi jina lake ni “Madharau;”matendo yake yamejaa majivuno ya ufidhuli wake.

25. Mvivu hufa kwa kutotimizwa tamaa zake,maana mikono yake milegevu haitaki kufanya kazi.

26. Mchana kutwa mwovu hutamani kupata kitu,lakini mwadilifu hutoa, tena kwa ukarimu.

27. Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza,huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya.

28. Shahidi mwongo ataangamia,lakini msikivu hawezi kunyamazishwa.

Methali 21