Methali 20:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Watu wengi hujivunia kuwa wema,lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?

7. Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu;watoto wake atakaowaacha watabarikiwa.

8. Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu,huupepeta uovu wote kwa macho yake.

9. Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu;mimi nimetakasika dhambi yangu?”

10. Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu,vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

11. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,kama tabia yake ni njema na aminifu.

12. Sikio lisikialo na jicho lionalo,yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.

Methali 20