Methali 20:17-25 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu,lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.

18. Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana;ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.

19. Mpiga domo hafichi siri,kwa hiyo mwepe mtu wa kuropoka.

20. Anayemlaani baba yake au mama yake,mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani.

21. Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni,haitakuwa ya heri mwishoni.

22. Usiseme, “Nitalipiza ubaya niliotendewa.”Mtegemee Mwenyezi-Mungu naye atakusaidia.

23. Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,na vipimo visivyo halali ni kitu kibaya.

24. Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi-Mungu;awezaje binadamu kujua njia ya kwenda?

25. Ni hatari kusema kwa mzaha “Usiahidi kumpa Mungu kitu bila kufikiri,la sivyo utaanza kusikitika baada ya nadhiri yako.”

Methali 20