1. Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu,na kuyathamini maagizo yangu;
2. ukitega sikio lako kusikiliza hekima,na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu;
3. naam, ukiomba upewe busara,ukisihi upewe ufahamu;
4. ukiitafuta hekima kama fedha,na kuitaka kama hazina iliyofichika;
5. hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu,utafahamu maana ya kumjua Mungu.
6. Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima;kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7. Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi,yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu.