1. Afadhali maskini aishiye kwa unyofu,kuliko mtu mpotovu wa maneno na mpumbavu.
2. Haifai mtu kuwa bila akili;mwenda harakaharaka hujikwaa.
3. Mtu akijiangamiza kwa upumbavu wake,huielekeza hasira yake dhidi ya Mwenyezi-Mungu.
4. Mali huvuta marafiki wengi wapya,lakini maskini huachwa bila rafiki.
5. Shahidi mwongo hataacha kuadhibiwa;asemaye uongo hataepa adhabu.
6. Watu wengi hujipendekeza kwa wakuu;kila mtu hutaka kuwa rafiki ya mtu mkarimu.
7. Maskini huchukiwa na ndugu zake;marafiki zake ndio zaidi: Humkimbia!Hata awabembeleze namna gani hatawapata.
8. Ajipatiaye hekima anaipenda nafsi yake;anayezingatia busara atastawi.
9. Shahidi mwongo hatakosa kuadhibiwa;asemaye uongo ataangamia.
10. Haifai kwa mpumbavu kuishi kwa anasa,tena ni vibaya zaidi mtumwa kuwatawala wakuu.