Methali 18:2-9 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Mpumbavu hapendezwi na busara;kwake cha maana ni maoni yake tu.

3. Ajapo mwovu huja pia dharau;pamoja na aibu huja fedheha.

4. Maneno yaweza kuwa chemchemi ya hekima;yenye kilindi kama bahari, kama kijito kinachobubujika.

5. Si vizuri kumpendelea mtu mwovu,na kumnyima haki mtu mwadilifu.

6. Maneno ya mpumbavu huleta ugomvi;kila anachosema husababisha adhabu.

7. Kinywa cha mpumbavu humwangamiza mwenyewe;mdomo wake ni mtego wa kumnasa yeye mwenyewe.

8. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo kitamu;ambacho hushuka moja kwa moja mpaka tumboni.

9. Mtu mvivu kazini mwakeni ndugu yake mharibifu.

Methali 18