Methali 18:13-24 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Kujibu kabla ya kusikilizani upumbavu na jambo la aibu.

14. Roho ya mtu huweza kustahimili ugonjwa,lakini ukiwa umevunjika moyo, utastahimilije?

15. Mtu mwenye akili hujipatia maarifa,sikio la mwenye busara hutafuta maarifa.

16. Zawadi humfungulia mtu milango;huweza kumfikisha mtu mbele ya mkuu.

17. Ajiteteaye kwanza huonekana msema kweli,mpaka hapo mpinzani wake atakapoanza kumhoji.

18. Kura hukomesha ubishi;huamua kati ya wakuu wanaopingana.

19. Ndugu aliyeudhiwa ni mgumu kuliko mji wa ngome;magomvi hubana kama makufuli ya ngome.

20. Maneno ya mtu yaweza kumshibisha;hutosheka kwa matokeo ya maneno yake.

21. Ulimi una nguvu ya kufanya hai na kuua;wanaopenda kuutumia watakula matunda yake.

22. Anayempata mke amepata bahati njema;hiyo ni fadhili kutoka kwa Mwenyezi-Mungu.

23. Maskini huomba kwa unyenyekevu,bali tajiri hujibu kwa ukali.

24. Marafiki wengi waweza kumwangusha mtu,lakini wapo marafiki waaminifu kuliko ndugu.

Methali 18