Methali 18:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Anayetafuta yake tu hujitenga na wenzake;hukasirika akipewa shauri lolote jema.

2. Mpumbavu hapendezwi na busara;kwake cha maana ni maoni yake tu.

3. Ajapo mwovu huja pia dharau;pamoja na aibu huja fedheha.

4. Maneno yaweza kuwa chemchemi ya hekima;yenye kilindi kama bahari, kama kijito kinachobubujika.

5. Si vizuri kumpendelea mtu mwovu,na kumnyima haki mtu mwadilifu.

Methali 18