Methali 17:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Kuanzisha ugomvi ni kama kufanya ufa kwenye bwawa;achana na ugomvi kabla haujafurika.

15. Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatiayote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

16. Ya nini mpumbavu kuwa na fedha mkononi kununulia hekima,wakati yeye mwenyewe hana akili?

17. Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote,ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu.

18. Si jambo la akili kuweka rehani,na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.

Methali 17