Methali 16:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Binadamu hupanga mipango yake,lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu.

2. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa,lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu.

3. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako,nayo mipango yako itafanikiwa.

4. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake;hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi.

5. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu;hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa.

6. Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi,kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu.

7. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu,huwageuza hata adui zake kuwa marafiki.

8. Afadhali mali kidogo kwa uadilifu,kuliko mapato mengi kwa udhalimu.

9. Mtu aweza kufanya mipango yake,lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake.

10. Mfalme huamua kwa maongozi ya Mungu;anapotoa hukumu hakosei.

Methali 16