Methali 15:26-33 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Mawazo ya mwovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,bali maneno mema humfurahisha.

27. Anayetamani faida ya ulanguzianaitaabisha jamaa yake,lakini achukiaye hongo ataishi.

28. Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu,lakini kinywa cha mwovu hububujika uovu.

29. Mwenyezi-Mungu yuko mbali na watu waovu,lakini yu karibu na watu wema kuwasikiliza.

30. Macho ya huruma hufurahisha moyo,habari njema huuburudisha mwili.

31. Mtu ambaye husikiliza maonyo mema,anayo nafasi yake miongoni mwa wenye hekima.

32. Anayekataa kufundishwa anajidharau mwenyewe,bali anayekubali maonyo hupata busara.

33. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni shule ya hekima;kabla ya kuheshimika ni lazima kuwa mnyenyekevu.

Methali 15