Methali 15:19-24 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Njia ya mvivu imesambaa miiba,njia ya mwaminifu ni wazi kama barabara kuu.

20. Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake,lakini mpumbavu humdharau mama yake.

21. Upumbavu ni furaha kwa mtu asiye na akili,lakini mwenye busara huchagua njia iliyo sawa.

22. Mipango huharibika kwa kukosa shauri,lakini kwa washauri wengi, hufaulu.

23. Kutoa jibu sahihi hufurahisha;neno lifaalo kwa wakati wake ni jema mno!

24. Njia ya mwenye hekima huelekea juu kwenye uhai,ili aepe kuingia chini kuzimu.

Methali 15