1. Kujibu kwa upole hutuliza hasira,lakini neno kali huchochea hasira.
2. Ulimi wa mwenye hekima hueneza maarifa,lakini watu wapumbavu hububujika upuuzi.
3. Macho ya Mwenyezi-Mungu huona kila kitu,humchunguza mtu mwema na mtu mbaya.
4. Ulimi mpole ni chanzo cha uhai,lakini uovu wake huvunja moyo.
5. Mpumbavu hudharau mafundisho ya baba yake,lakini anayekubali maonyo ana busara.
6. Nyumbani mwa mwadilifu mna wingi wa mali,lakini mapato ya waovu huishia na balaa.