Methali 13:20-25 Biblia Habari Njema (BHN)

20. Anayeandamana na wenye hekima hupata hekima,lakini anayejiunga na wapumbavu atapata madhara.

21. Watendao dhambi huandamwa na balaa,lakini waadilifu watatuzwa mema.

22. Mtu mwema huwaachia urithi uzao wake,lakini mali ya mwenye dhambi imerundikiwa waadilifu.

23. Shamba la maskini hutoa mazao mengi,lakini bila haki hunyakuliwa.

24. Asiyemwadhibu mtoto wake hampendi;lakini ampendaye mwanawe humrudi mapema.

25. Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza,lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa.

Methali 13