Methali 13:14-20 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Mafundisho ya wenye hekima ni chemchemi ya uhai;humwezesha mtu kuiepa mitego ya kifo.

15. Kuwa na akili huleta fadhili,lakini njia ya waovu ni ya taabu

16. Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili,lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake.

17. Mjumbe mbaya huwatumbukiza watu taabuni,lakini mjumbe mwaminifu huleta nafuu.

18. Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho,lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa.

19. Inafurahisha upatapo kile unachotaka,kwa hiyo wapumbavu huchukia kuepa uovu.

20. Anayeandamana na wenye hekima hupata hekima,lakini anayejiunga na wapumbavu atapata madhara.

Methali 13