1. Mtoto mwenye hekima husikia maagizo ya baba yake,lakini mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2. Mtu mwema hupata mema kutokana na maneno yake,lakini wadanganyifu huishi kwa ukatili.
3. Achungaye mdomo wake huyahifadhi maisha yake,anayeropoka ovyo hujiletea maangamizi.
4. Mvivu hutamani lakini hapati chochote,hali mwenye bidii hujaliwa riziki kwa wingi.
5. Mwadilifu huuchukia uongo,lakini mwovu hutenda kwa aibu na fedheha.
6. Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu,lakini dhambi huwaangusha waovu.
7. Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu;wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.
8. Fidia ya mtu ni mali yake,lakini maskini hana cha kutishwa.
9. Mwadilifu hungaa kama taa iwakayo vizuri,lakini waovu ni kama taa inayozimika.
10. Kiburi husababisha tu ugomvi,lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima.