23. Mwenye busara huficha maarifa yake,lakini wapumbavu hutangaza upumbavu wao.
24. Kuwa na bidii kutampa mtu cheo,lakini uvivu utamfanya mtumwa.
25. Wasiwasi moyoni humkosesha mtu raha,lakini neno jema humchangamsha.
26. Mtu mwadilifu huuepa uovu,lakini njia ya waovu huwapotosha wenyewe.
27. Mwindaji mvivu hatapata anachowinda,lakini mwenye bidii atafanikiwa.
28. Uadilifu ni njia ya uhai,lakini uovu huongoza katika mauti.