Methali 12:21-27 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Waadilifu hawapatwi na jambo lolote baya,lakini waovu wamejaa dhiki.

22. Midomo isemayo uongo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,lakini watu waaminifu ni furaha yake.

23. Mwenye busara huficha maarifa yake,lakini wapumbavu hutangaza upumbavu wao.

24. Kuwa na bidii kutampa mtu cheo,lakini uvivu utamfanya mtumwa.

25. Wasiwasi moyoni humkosesha mtu raha,lakini neno jema humchangamsha.

26. Mtu mwadilifu huuepa uovu,lakini njia ya waovu huwapotosha wenyewe.

27. Mwindaji mvivu hatapata anachowinda,lakini mwenye bidii atafanikiwa.

Methali 12