Methali 10:26-32 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Kama ilivyo siki kwa meno au moshi machoni,ndivyo alivyo mvivu kwa bwana wake.

27. Kumcha Mwenyezi-Mungu hurefusha maisha,lakini miaka ya waovu itakuwa mifupi.

28. Tumaini la mwadilifu huishia kwenye furaha,lakini tazamio la mwovu huishia patupu.

29. Mwenyezi-Mungu ni ngome ya wanyofu,lakini watendao maovu atawaangamiza.

30. Waadilifu kamwe hawataondolewa nchini,lakini waovu hawatakaa katika nchi.

31. Kinywa cha mwadilifu hutoa mambo ya hekima,lakini ulimi wa mtu mbaya utakatiliwa mbali.

32. Midomo ya waadilifu hujua yanayokubalika,lakini vinywa vya waovu husema tu maovu.

Methali 10