26. “Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.
27. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena anguko hilo lilikuwa kubwa.”
28. Yesu alipomaliza kusema maneno hayo, umati wa watu ukashangazwa na mafundisho yake.
29. Hakuwa kama waalimu wao wa sheria, bali alifundisha kwa mamlaka.