Mathayo 4:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”

8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,

9. akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

10. Hapo, Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Imeandikwa:‘Utamwabudu Bwana Mungu wakona kumtumikia yeye peke yake.’”

11. Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.

12. Yesu aliposikia kwamba Yohane ametiwa gerezani alikwenda Galilaya.

13. Aliondoka Nazareti, akaenda Kafarnaumu, mji ulio kando ya bahari ya Genesareti, mpakani mwa wilaya za Zebuluni na Naftali, akakaa huko.

14. Ndivyo lilivyotimia lile neno lililosemwa kwa njia ya nabii Isaya:

15. “Nchi ya Zebuluni na nchi ya Naftali,kuelekea baharini ngambo ya mto Yordani,Galilaya, nchi ya watu wa mataifa!

16. Watu waliokaa gizaniwameona mwanga mkubwa.Nao walioishi katika nchi ya giza na kivuli cha kifo,mwanga umewaangazia!”

17. Tangu wakati huo Yesu alianza kuhubiri akisema, “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekariia!”

Mathayo 4