Mathayo 4:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

4. Yesu akamjibu, “Imeandikwa:‘Mtu haishi kwa mkate tu,ila kwa kila neno asemalo Mungu.’”

5. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,

6. akamwambia, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa:‘Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako;watakuchukua mikononi mwao,usije ukajikwaa kwenye jiwe.’”

7. Yesu akamwambia, “Imeandikwa pia:‘Usimjaribu Bwana, Mungu wako.’”

8. Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,

9. akamwambia, “Hivi vyote nitakupa kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

Mathayo 4