Mathayo 26:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake,

2. “Mnajua kwamba baada ya siku mbili tutakuwa na sikukuu ya Pasaka, na Mwana wa Mtu atatolewa ili asulubiwe.”

3. Wakati huo makuhani wakuu na wazee wa watu walikutana pamoja katika ukumbi wa Kayafa, kuhani mkuu.

4. Wakashauriana jinsi ya kumtia Yesu nguvuni kwa hila wamuue.

5. Lakini wakaamua jambo hilo lisifanyike wakati wa sikukuu, kusije kukatokea ghasia kati ya watu.

6. Yesu alipokuwa Bethania, nyumbani kwa Simoni, aitwaye Mkoma,

7. mama mmoja aliyekuwa na chupa ya alabasta yenye marashi ya thamani kubwa, alimjia pale mezani alipokuwa amekaa kula chakula, akammiminia hayo marashi kichwani.

Mathayo 26