Mathayo 25:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Wakati huo, ufalme wa mbinguni utafanana na wasichana kumi waliochukua taa zao, wakaenda kumlaki bwana arusi.

2. Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara.

3. Wale wapumbavu walichukua taa zao, lakini hawakuchukua akiba ya mafuta.

4. Lakini wale wenye busara walichukua mafuta katika chupa pamoja na taa zao.

5. Kwa kuwa bwana arusi alikawia kuja, wale wasichana wote walisinzia, wakalala.

6. Usiku wa manane kukawa na kelele: ‘Haya, haya! Bwana arusi anakuja; nendeni kumlaki.’

Mathayo 25