6. Mtasikia juu ya vita na fununu za vita; lakini msifadhaike, maana hayo hayana budi kutokea, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
7. Taifa moja litapigana na taifa lingine; ufalme mmoja utapigana na ufalme mwingine. Hapa na pale patakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi.
8. Yote hayo ni kama mwanzo wa maumivu ya kujifungua mtoto.
9. “Kisha watawatoeni ili mteswe na kuuawa. Mataifa yote yatawachukieni kwa sababu ya jina langu.
10. Tena, wengi wataiacha imani yao, watasalitiana na kuchukiana.
11. Watatokea manabii wengi wa uongo watakaowapotosha watu wengi.
12. Kwa sababu ya ongezeko la uhalifu, upendo wa watu wengi utafifia.
13. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
14. Ila, kabla ya mwisho kufika, hii Habari Njema ya ufalme wa Mungu itahubiriwa ulimwenguni kote kama ushuhuda kwa mataifa yote.