35. Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi. Naam, tangu kumwagwa damu ya Abeli ambaye hakuwa na hatia, mpaka ile ya Zakaria, mwana wa Barakia, ambaye mlimuua hekaluni kati ya patakatifu na madhabahu.
36. Nawaambieni kweli, kizazi hiki kitapata adhabu kwa sababu ya mambo haya.
37. “Yerusalemu! Ee Yerusalemu! Unawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya watoto wako kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.
38. Haya basi, nyumba yako itaachwa mahame.
39. Nakuambia, hutaniona tena mpaka wakati utakaposema:‘Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”