1. Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake,
2. “Waalimu wa sheria na Mafarisayo wana mamlaka ya kufafanua sheria ya Mose.
3. Kwa hiyo shikeni na kutekeleza chochote watakachowaambieni. Lakini msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyahubiri.
4. Hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.
5. Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa tepe zenye maandishi ya sheria juu ya panda la uso na mikononi na hupanua pindo za makoti yao.
6. Hupenda nafasi za heshima katika karamu na viti vya heshima katika masunagogi.
7. Hupenda kusalimiwa kwa heshima sokoni na kupendelea kuitwa na watu: ‘Mwalimu.’