8. Umati mkubwa wa watu wakatandaza nguo zao barabarani, na watu wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani.
9. Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaza sauti:“Sifa kwa Mwana wa Daudi!Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!Sifa kwa Mungu juu!”
10. Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu, mji wote ukajaa ghasia. Watu wakawa wanauliza, “Huyu ni nani?”