Mathayo 21:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Yesu na wanafunzi wake walipokaribia Yerusalemu na kufika Bethfage katika mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,

2. akawaambia, “Nendeni hadi kijiji kilicho mbele yenu na mtamkuta punda amefungwa na mtoto wake. Wafungueni mkawalete kwangu.

3. Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji,’ naye atawaachieni mara.”

4. Jambo hili lilifanyika ili yale yaliyosemwa na nabii yatimie:

5. “Uambieni mji wa Siyoni:Tazama, Mfalme wako anakujia!Ni mpole na amepanda punda,mwanapunda, mtoto wa punda.”

6. Hivyo, wale wanafunzi walikwenda wakafanya kama Yesu alivyowaagiza.

7. Wakamleta yule punda na mtoto wake, wakatandika nguo zao juu yao na Yesu akaketi juu yake.

8. Umati mkubwa wa watu wakatandaza nguo zao barabarani, na watu wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani.

Mathayo 21