Mathayo 15:34-39 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakamjibu, “Saba na visamaki vichache.”

35. Basi, Yesu akawaamuru watu wakae chini.

36. Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.

37. Wote wakala, wakashiba. Kisha wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu saba.

38. Hao waliokula walikuwa wanaume 4,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

39. Basi, Yesu akawaaga watu, akapanda mashua, akaenda katika eneo la Magadani.

Mathayo 15