55. Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda?
56. Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi, amepata wapi haya yote?”
57. Basi, wakawa na mashaka naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”
58. Kwa hiyo, hakutenda miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao.