Mathayo 13:2-12 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashuani, akaketi. Watu wote walisimama kwenye ukingo wa ziwa,

3. naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano.“Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.

4. Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.

5. Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Zikaota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.

6. Jua lilipochomoza, ziliteketea; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.

7. Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga.

8. Nyingine zilianguka penye udongo mzuri, zikaota, zikazaa: Nyingine punje mia, nyingine sitini na nyingine thelathini.

9. Mwenye masikio na asikie!”

10. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwuliza, “Kwa nini unasema na watu kwa mifano?”

11. Yesu akawajibu, “Nyinyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujaliwa.

12. Maana, aliye na kitu atapewa na kuzidishiwa; lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.

Mathayo 13