Mathayo 13:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku hiyohiyo, Yesu alitoka katika ile nyumba, akaenda na kuketi kando ya ziwa.

2. Makundi makubwa ya watu yalimzunguka hata Yesu akapanda mashuani, akaketi. Watu wote walisimama kwenye ukingo wa ziwa,

3. naye Yesu akawaambia mambo mengi kwa mifano.“Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.

4. Alipokuwa akipanda mbegu, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.

Mathayo 13