21. Atajifungua mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu, kwa kuwa yeye ndiye atakayewaokoa watu wake katika dhambi zao.”
22. Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:
23. “Bikira atachukua mimba,atamzaa mtoto wa kiume,nao watampa jina Emanueli”(maana yake, “Mungu yuko nasi”).
24. Hivyo, Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo alivyomwambia, akamchukua mke wake nyumbani.
25. Lakini hakulala naye hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.