Matendo 2:22-28 Biblia Habari Njema (BHN)

22. “Wananchi wa Israeli, sikilizeni maneno haya! Yesu wa Nazareti alikuwa mtu ambaye mamlaka yake ya kimungu yalithibitishwa kwenu kwa miujiza, maajabu na ishara Mungu alizofanya kati yenu kwa njia yake, kama mnavyojua.

23. Kufuatana na mpango wake mwenyewe Mungu alikwisha amua kwamba Yesu angetiwa mikononi mwenu; nanyi mkamuua kwa kuwaachia watu wabaya wamsulubishe.

24. Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, akamwokoa katika maumivu ya kifo kwa maana haingewezekana kabisa kifo kimfunge.

25. Maana Daudi alisema juu yake hivi:‘Nilimwona Bwana mbele yangu daima;yuko nami upande wangu wa kulia hata sitatikisika.

26. Kwa hiyo, moyo wangu ulifurahi;tena nilipiga vigelegele vya furaha.Mwili wangu utakaa katika tumaini,

27. maana hutaiacha roho yangu kuzimu,wala kumruhusu mtakatifu wako aoze.

28. Umenionesha njia za uhai,umenijaza furaha kwa kuwako kwako!’

Matendo 2